<
>
Download

Übersetzung
Literaturwissenschaft

The Aga Khan Academy, Mombasa

AKA

Kristina A. ©
2.40

0.08 Mb
sternsternsternsternstern_0.2
ID# 79916







DP1-KISWAHILI BW. NYAGAH



DP 1

MITIHANI

SWAHILI B – HIGHER/STANDARD LEVEL

MUDA: MASAA 2


  1. INSHA

Kamilisha kazi hii kwa maneno kati ya 250 na 400.


SWALI: Wewe kama mwanafunzi katika shule yako umeshangazwa na namna wanafunzi wenzako wanavyolalamika kila wakati kuhusu hali ya chakula, maji, takataka na wale ndege aina ya kunguru. Mwalimu Mkuu amekuuliza uwahutubie wanafunzi hawa kuhusu maswala haya na hasa namna ya kuyasuluhisha. Andika hotuba hiyo.


Wageni waalikwa, wazazi, Mwalimu Mkuu, walimu na wanafunzi wenzangu; hamjambo?
Jina langu ni . Mimi ni mwanafunzi wa daraja la Diploma ya mwaka wa kwanza, katika shule ya Aga Khan Academy, Mombasa. Ni mmojawapo wa viongozi wa wanafunzi humu shuleni.

Ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa fursa hii niliopewa kusimama mbele yenu ili kuwanzungumzia kuhusu hali ya chakula, maji, takataka, bila kusahau hawa ndege wasumbufu wanaoitwa kunguru. Pia, nawashukuru waandalizi wa mkutano huu unaotuleta pamoja ili kutatua maswala haya yanayotukumba.

Hii inaonyesha imani mliyo nayo kwetu sisi kama wanafunzi kuweza kuchangia katika suluhisho la shida zetu.

Mimi nikiwakilisha wanafunzi katika shule hii, nimepokea malalamishi kadha wa kadha kuhusu hali ya chakula, maji, takataka na kunguru. Maswala haya ni muhimu sana katika afya yetu. Kwanza kabisa, ningependa kuzungumzia swala la uharibifu wa chakula shuleni. Ningependa kutambua kwamba shule yetu inaandaa chakula cha hali ya juu na aina mbalimbali.

Chakula hiki kina madini kama; protini, wanga, vitamini zinazotokana na mboga na matunda. Lakini, wanafunzi wanalalamika kuwa hakuna vyakula vya kisasa kama vile piza, baga na vyakula vya chokoleti na soda. Lakini ningependa kuwahamasisha wanafunzi wenzangu kuhusu umuhimu wa vyakula tunavyokula hapa shuleni kwa sababu vina kila madini yanayohitajika katika kukua kwa miili yetu.

Kwa upande mwingine, kuna hili swala la uharibifu wa chakula unaotokana na chakula kingi kutupwa kwenye mapipa ya takataka. Kwa maoni yangu, ningependa kuwashauri wanafunzi wenzangu muwe makini sana katika kutumia chakula unachohitaji. Tukisuluhisha hili swala, tutakuwa pia tumesuluhisha swala la takataka hapa shuleni.

Kusema kweli, takataka nyingi zinatokana na vyakula au vinywaji tunavyotumia na hapa ningependa kutoa pendekezo ili tuwe na mapipa mbalimbali ya kuwekea mikebe, karatasi na vyakula. Hapa ningeomba tuwe na mapipa mengi hasa kwenye maeneo ya duka na pia uwanjani. Hii itasaidia kutupa taka zetu mahali tunapochezea au tunaponunua vyakula vyetu.

Mimi naonelea tukifanya hivi, tutaweza pia kujali mazingira yetu wenyewe kwani usipoziba ufa, utajenga ukuta. Ni ombi langu kwa Mwalimu Mkuu, afuatilie mambo haya kwa karibu.

Vile vile, nimepokea malalamishi kuhusu uhaba wa chupa za maji mara kwa mara. Tukumbuke kwamba, maji ni uhai! Mimi ningependa kutilia mkazo, swala la kuongeza idadi ya vituo vya maji hapa shuleni kwa sababu mara nyingi, utakuta hakuna vituo vya maji mahali ambapo vingefaa kuwa.

Hatimaye, kuna swala la kunguru! Ndege hawa wanatukera sana hasa tunapokula mahali popote pale. Wanabakura vyakula vyetu hata mkononi. Sijui swala hili mtaliangalia kivipi kama shule ili tuwe na usalama tunapokula hata chini ya mabanda. Labda, ningependekeza kuwepo na watu wenye panda au manati ili kuwatishia ndege hawa hasa katika maeneo tunapokula chakula.

Nikimalizia, acha niseme kuwa nina imani kubwa na usimamizi wa shule yetu kwamba wataangalia maswala haya kwa karibu na kuboresha maisha yetu hapa shule. Natoa shukrani zangu tena kwenu nyote mliokaa na kunisikiliza kwa makini.


  1. MATUMIZI YA LUGHA

JIBU MASWALI YOTE

  1. Fuata maagizo uliyopewa.(Alama 4)


  1. Amepachika mkoba wake kwapani.(Andika kwa wingi).


Wamepachika mikoba yao makwapani.


  1. Wezi wa mabavu wangeshikwa, wangeuliwa na umati wa watu(Kanusha). - negate


Wezi wa mabavu wasingeshikwa wasingeuliwa na umati wa watu.


  1. Juma aliniuliza kama nilikuwa nimechukua kitabu chake.(Andika kwa usemi halisi). – direct speech


Umechukua kitabu changu?”, Juma aliniuliza.


  1. Waimbaji hao walipanda juu ya majukwaa.(Geuza kwa umoja).- singular


Mwimbaji huyo alipanda juu ya jukwaa.


  1. Sahihisha sentensi zifuatazo.(Alama 2)



Ngamia ambao wameuzwa ni wetu.


  1. Kitabu aliyesoma ina picha mzuri sana.


Kitabu alichosoma kina picha nzuri sana.


  1. Tunga sentensi ukitumia maneno yafuatayo.(Alama 4).


  1. Isitoshe


Isitoshe, vituo hivi mara nyingi huwa havina maji baridi kwa sababu friji huwa zimeharibika na inachukua muda mrefu kwa shule kuzirekebisha.

  1. Licha ya (despite/ in spite of)


Licha ya kumuonya asivuke barabara, yeye alivuka tu.


  1. Angaa (at least)


Ningependa unisaidie na vitabu vya kusoma, angaa viwili.


  1. Maadam (since/because – causative connotation)


Maadam umeniuliza, nitakupa jibu.


| | | | |
Tausche dein Hausarbeiten